Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

YANGA YATAKIWA KUMUWASILISHA MAXIMO TFF.





                 kocha mkuu wa Yanga Marcio Maximo na msaidizi wake.

Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
YANGA SC wametakiwa kuwasilisha jina la kocha wao mpya, Mbrazil Marcio Maximo na wasaidizi wake.
Hiyo imo katika agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuzitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha orodha ya watendaji wa mabenchi yao ya ufundi yakiongozwa na Kocha Mkuu.

Ni wajibu wa klabu kuhakikisha zinatekeleza maagizo hayo kwani ni matakwa ya Kanuni za VPL na zile za FDL.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu wakati ile ya FDL inatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment