Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 31, 2014

ANDY MURRY ASEMA YUPO FITI KUMKABILI JO-WILFRED TSONG US OPEN 2014.



                                       Andy Murry.

Wakati akijiandaa kumkabili Jo-Wilfred Tsonga katika  michuano ya wazi ya Marekani mcheza tenisi Andy Murry amesema anaamini atafanya vyema licha ya kusumbuliwa na maumivu kwa siku kadhaa hivi sasa.
Murry ambaye amefanikiwa kuingia mzunguko wanne wa mashindano hayo baada ya kumshinda Andrey Kuznetsov jana jumamosi kwa seti 6 kwa1,7 kwa 5,4 kwa 6 na 6 kwa 2 amesema ushindi huo umedhihirisha kwamba amepona vyema.
Akizungumza baada ya ushindi huo Murry anayeshika nafasi ya 9 kwa ubora wa mchezo huo duniani upande wa wanaume amebainisha kwamba uwezo aliouonesha hapo jana ulikuwa ni wa hali ya juu lakini akiahidi kuongeza kasi zaidi.
Michuano hiyo ya wazi imeingia katika wiki ya pili ambapo wachezaji mbalimbali wa kiume na wakakike duniani wanapambana nchini Marekani kuwania ubingwa kwa mwaka huu.

                              Mkule.blogsport.com

SUPER MARIO BALOTELLI ATEMWA KATIKA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ITALIA.



                    Kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte.

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ametangaza kikosi chake cha kwanza tangu apewe jukumu la kukifundisha kikosi hicho  huku kwenye orodha hiyo jina la mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Baloteli likikosekana.

Kikosi hicho ambacho ni chakwanza tangu Conte achukue nafasi ya Cesare Prandelli aliyejiuzulu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Uruguay kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu zilizofanyika nchini Brazil.

Uteuzi wa kikosi hicho ni kwaajili ya mchezo wa kirafiki na Uholanzi utakaochezwa septemba 4 mwaka huu kabla ya kuikabili Norway siku tano baadae kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2016.

Licha ya Balotelli kuachwa kocha Antonio Conte amewaita mlinda mlango mkongwe Jiji Buffon na wachezaji wengine kama , Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci, Daniele De Rossi na Claudio Marchisio  wote wamejumuishwa pamoja na  Ciro Immobile, Simone Zaza na Sebastian Giovinco.

Kikosi kamili cha Italia hiki hapa:-


Goalkeepers: Gianluigi Buffon (Juventus), Daniele Padelli (Torino), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris Saint Germain);

Defenders: Davide Astori (Roma), Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Gabriel Paletta (Parma), Andrea Ranocchia (Inter);

Midfielders: Antonio Candreva (Lazio), Matteo Darmian (Torino), Daniele De Rossi (Roma), Mattia De Sciglio (Milan), Alessandro Florenzi (Roma), Emanuele Giaccherini (Sunderland), Christian Maggio (Napoli), Claudio Marchisio (Juventus), Marco Parolo (Lazio), Manuel Pasqual (Fiorentina), Andrea Poli (Milan), Marco Verratti (Paris Saint Germain);

Attackers: Mattia Destro (Roma), Stephan El Shaarawy (Milan), Sebastian Giovinco (Juventus), Ciro Immobile (Borussia Dortmund), Pablo Osvaldo (Inter), Simone Zaza (Sassuolo).



                                   Mkule.blogsport.com

KAMATI ZA UFUNDI, MASHINDANO NA VIJANA ZATANGAZWA.




                              Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu.

  Wajumbe Wenza wa Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendelo ya Michezo), Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji, wanapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wanaYANGA, wameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji ya YANGA zifuatazo:

1) KAMATI YA UFUNDI
Wajumbe:

 1)  Duduma, Nassoro
 2)  Lamlembe, Roger
 3)  Malulu, Pascal 
 4)  Msolla, Peter
 5)  Zangira, Steve

2) KAMATI YA SOKA YA VIJANA NA WANAWAKE
Wajumbe:

1) Katwila, Shaban
2) Kabisa, Jessica (Advocate)
3) Mazwile, Isack
4) Mwita, George
5) Tembele, Ally Mayay

3) KAMATI YA MASHINDANO 
Wajumbe:

1)  Cheyo, Magembe      
2)  Didi, Ibrahim                  
3)  Hussein, Ndama Risasi      
4)  Katabalo, Moses             
5)  Katunzi, Mudhamiri        
6)  Kihanga, Pascal 
7)  Kingo, Ray Shauri
8)  Kleb, Abdallah Bin
9)  Luhago, David
10) Lukumay, Samwel
11) Macha, Innocent 
12) Maige, Jackson 
13) Mahende, Mugaya   
14) Makay, Sule       
15) Malebo, Michael  
16) Malume, Paul 
17) Matata 
18) Mbise, Anandumi Timothy 
19) Mlangwa, David 
20)  Mogha, John  
21) Mutaboyerwa, Joseph John
22) Ntimizi, Said
23) Nyambaya, Lameck
24) Nyika, Hussein
25) Nyumbamkaly,
26) Ramadhan, Fulgence 
27) Rashid, Ahmed    
28) Suleman, Majid    
29) Tenga, Frank  
30) Tindwa, Beda
31) Zakaria, Dr.      
   
Ifahamikekwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamatiza YANGA zilizotajwa hapo juu.

Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji Wajumbe Wenza wa Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendelo ya Michezo) watakuwa Wenyekiti Wenza wa Kamati zilizotajwa hapo juu.

Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze ketenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA.

(YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO)

(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU WA YANGA.

                              Mkule.blogsport.com