Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 31, 2014

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ.





                                     Arturo Vidal.
Taarifa zilizoifikia Mkule.blogsport.com zimearifu kuwa mshambuliaji wa Juventus Turin ya Italia Arturo Vidal amefaulu vipimo vya afya tayari kwakutua rasmi Manchester United ya nchini England.
Tayari Vidal mwenye umri wa miaka 27 ameahidiwa kulipwa kiasi cha paundi laki mbili kwa wiki cha mshahara  na miamba hao wa soka wa nchini Uingereza.

 Hapa Vidal akiwasili katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United Carrington, kwakufanyiwa vipimo vya afya.

Endapo dili hili linalofanyika kwa siri litakamilika Vidal huenda akapewa jezi namba 7 ambayo imewahi kuvaliwa na wachezaji mbalimbali kwenye timu hiyo akiwemo Cristiano Ronaldo,David Bekham,Antonio Valencia,Michael Owen,George Best na Eric Cantona.

Kwasasa jezi hiyo haina mtu.


Habari zaidi zitaendelea kukujia hapahapa kupitia 

                            Mkule.blogsport.com

NADAL KUKAA NJE WIKI MBILI HADI TATU.





                                        Rafael Nadal.

Mcheza Tenisi Rafael Nadal anataraji kukaa nje ya uwanja kwa majuma matatu baada ya kuuumia  kifundo cha kiganja wakati akifanya mazoezi  jumanne ya wiki hii.

Kuumia kwa mchezaji huyo anayeshika nafasi ya pili kwa ubora wa Tenisi duniani kumekuja ikiwa ni majuma kadhaa  kabla ya kuanza kwa mashindano ya wazi ya marekani yanayotaraji kufanyika mjini New York Marekani.

Nadal mwenye umri wa miaka 28 kwasasa atashindwa kutetea mataji yake ya michuano ya Toronto  na Cincinnati mwaka huu huku ikielezwa atakuwa tayari kurejea uwanjani kwenye michuano ya wazi ya Marekani inayoanza  tarehe 25 ya mwezi wa nane.

Mchezaji huyo amethibitisha kuwa ameumia kifundo cha mkono wake wa kulia wakati akiwa mazoezini na anataraji kupatiwa matibabu   na madaktari wake yatakayomfanya atumie majuma mawili hadi matatu ili kupona.

                     Mkule.blogsport.com

MOURINHO: JEURI YA LUKAKU NDIYO ILIYONIFANYA NIMUUZE.





                                Jose Mourinho.
Baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Chelsea Romelu Lukaku   kujiunga na Everton kocha Jose Mourinho amesema mchezaji huyo hakuwa tayari kupigania namba kwenye kikosi hicho cha jijini London.
Mourinho ameeleza sababu ya kuruhusu mchezaji huyo yaia wa Ubelgiji kuondoka Stanford Bridge kuwa Lukaku alitaka kuchezea Chelsea na awe chaguo la kwanza jambo ambalo ni gumu kwenye kikosi chake.
Kocha huyo raia wa Ureno  amezidi kutetea uamuzi wa kumuuza nyota huyo kwakusema baada ya Everton kupeleka dau zuri wamelazimika kummuuza mchezaji huyo ili klabu inufaike kwa kupata fedha za kuwasaidia.
Lukaku ambaye amejiunga na Everton maarufu kama Toffiz kwa uhamisho ulioweka rekodi kwa wachezaji wenye umri wa miaka 21 alifunga magoli 15 msimu uliopita wa ligi katika klabu hiyo akitokea Chelsea kwa mkopo.
                        Mkule.blogsport.com

STARS YATUA SALAMA AFRIKA YA KUSINI.



                              Kikosi cha Taifa Stars.
 
Na Boniface Wambura, JOHANNESBURG
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.


Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).
                         Mkule.blogsport.com

Wednesday, July 30, 2014

YAYA:NITAENDELEA KUWEPO MAN CITY KADRI ITAKAVYOWEZEKANA.



Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City Yaya Toure amebainisha kuwa anataka kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kadri ya itakavyowezekana.

 
Yaya Toure. 


Yaya mwenye umri wa miaka 31 amesema anafuraha kubakia kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya England na hasa baada ya kujiunga na timu hiyo inayojiandaa na msimu mpya wa 2014-2015.

kiungo huyo ambaye hapo awali alikuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na PSG ya Ufaransa amewataka mashabiki wa Manchester City kutoamini maneno yasiyotoka kwenye kinywa chake lakini yatakayozungumzwa na wakala wake ni ya kweli.

Toure ambaye ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Enfglannd msimu uliopita amesema anajisikia furaha kuungana na wenzaje kwenye maandalizi ya msimu mpya chini ya kocha Manuel Pellegrini.

                        Mkule.blogsport.com