Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 23, 2014

MARTINO AWAITA MESSI, DI MARIA NA KUN AGUERO KUIVAA BRAZIL MWEZI UJAO.



                     Kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina Reardo Martino


Kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina Reardo Martino amewajumuisha nyota hatari wa nchi hiyo kwenye kikosi kitakachoikabili Brazil kwenye mchezo wa Gillette  Superclasico de las America mwezi ujao mjini Beijing.
Katika orodha hiyo kocha huyo amewaita washabuliaji Leonel Messi ,Sergio Aguero  na kiungo Angel Di Maria tayari kwa mpambano huo utakaochezwa tarehe 10 ya mwezi ujao katika uwanja wa Bird Nest.
Katika orodha ya wachezaji walioitwa na kocha Gerardo Martino wamo nyota wa Benfica Nicolas Gaitan,kiungo wa Juventus Roberto Pereyra na mlinzi wa klabu ya  Villarreal ya Hispania Mateo Musacchio.
Michuano ya Superclasico de las America imerejeshwa mwaka 2011 baada ya kutofanyika kwa miaka 35 kabla ya mwaka jana mashindano ya Confederations Cup kufutwa na shirikisho la soka katika bara la Amerika ya kusini.
Kikosi kizima cha Argentina;-

walindamilango: Sergio Romero, Nahuel Guzman.
walinzi: Marcos Rojo, Federico Fernandez, Pablo Zabaleta, Martin Demichelis, Mateo Musacchio, Santiago Vergini.
Viungo : Javier Mascherano, Lucas Biglia, Javier Pastore, Roberto Pereyra, Angel Di Maria, Erik Lamela, Enzo Perez, Nicolas Gaitan.
washambuliaji: Lionel Messi, Gonzalo Higuain, Sergio Aguero.
                               Mkule.blogsport.com

SANTOS KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA URENO.



                                  Fernando Santos kocha mpya wa timu ya taifa ya Ureno.

Shirikisho la soka nchini Ureno FRF limemtangaza Fernando Santos kuwa kocha mpya wa timu yao ya taifa  kuchkua mikoba ya Paulo Bento aliyejiuzulu hivi karibuni  baada ya kufungwa na Albania kwenye mchezo wa kufuzu mataifa ya Ulaya EURO 2016.
Santos ambaye ni kocha wa zamani wa vilabu vya Fc Port na Benfica  ameifundisha timu ya taifa ya Ugiriki kwa miaka 4  na kuiwezesha kufika nusu fainali ya Euro 2012 huku akiivusha nchi hiyo hatua ya 16 bora kwenye kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil kabla ya kutolewa kwa matuta na Costa Rica.
Ureno  inataraji kucheza mchezo wa kirafiki na Ufaransa October 11 mjini Paris kabla ya kusafiri kuivaa Denmark  katika raundi ya pili ya kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya siku tate baadae.
Santos aliachia kibarua cha kuifundisha Ugriki siku mmoja baada ya kuondoshwa kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu  kabla ya mazungumzo ya kupewa mkataba  mkataba mpya kufanyika.
                             Mkule.blogsport.com

Monday, September 22, 2014

GOLI LA LAMPARD LALETA MAAFA NCHINI UGANDA.



                      Musana Fahad mwenye jezi ya kijani enzi za uhai wake.

 Shirikishon la soka nchini Uganda FUFA limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji Musana Fahad anayeichezea timu ya Simba Fc inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo UPL kilichotokea jana jioni muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Chelsea na Manchester City.

Musana mwenye umri wa miaka 24 kifo chake kimetajwa kutokea muda mchache baada ya kiungo wa Manchester City Frank Lampard kufunga goli la kusawazisha kwa mpira wa adhabu  na kufanya matokeo yawe goli 1 kwa 1.

Kifo cha mchezaji huyo ambaye imeelezwa kuwa ni shabiki mkubwa wa Chelsea kimehusishwa na mshtuko alioupata nyota huyo  kwakuwa jana asubuhi alikuwa mzima wa afya na alifanya mazoezi na timu yake ya Simba fc chini ya kocha Fred Kajoba.

Imeelezwa kuwa kabla ya  mchezaji huyo kupatwa na mauti alikimbizwa Hospitali ya Bombo iliyopo nchini humo na taraibu za mazishi yake zinafanywa na klabu yake wakishirikiana na familia ya marehemu.

                     Mkule.blogsport.com

KIBARUA CHA LAURENT BLANC KIPO SALAMA ASISITIZA RAIS WA PSG.



                 Rais wa PSG  Nasser Al-Khelaifi wakati akimtambulisha Laurent Blanc.

Licha ya PSG kuanza vibaya msimu huu wa ligi kuu ya Ufaransa rais wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi amesema kibarua cha kocha mkuu Laurent Blanc kamwe hakipo hatarini.

Akizungumza baada ya PSG kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1 na Olympique Lyonnais kwenye uwanja wake wa nyumbani rais huyo amesema wataendelea kuwa na kocha huyo hadi mwisho wa msimu pamoja na mwanzo mbaya walioanza nao.

Pamoja na kukiri kiwango chao cha sasa sio kile kilichotarajiwa amebainisha kwamba ni lazima wapambane kwa nguvu kila siku  ili kuwa kwenye kiwango kizuri na wanahakika ya kutimiza malengo ya msimu huu.

Rais huyo amesistiza kuwa mwenendo wa timu hiyo hivi sasa  unawakera wachezaji viongozi na wafanya kazi wote hivyo wote kwa pamoja watahakikisha wanacheza vyema michezo inayo fuata ikiwezo wa jumatano ya wiki hii ili kurudi katika kasi yao.

                                 Mkule.blogsport.com

Wednesday, September 17, 2014

QUEIROZ AONGEZA MKATANA WA KUIONOA TIMU YA TAIFA YA IRAN.



                                         Carlos Queiroz.

Kocha wa zamani wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Carlos Queiroz amefikia makubaliano ya kuiongeza mkataba   mpya wa miaka minne kuendelea kuifundisha timu ya taifa ya Iran.
Kocha huyo ambaye aliiongoza Iran mwaka huu kwenye fainali za kombe la dunia  nchini Brazil  alikuwa kwenye hatihati ya kuongeza mkataba mpya kwakile kilichoelezwa hakuwa na maelewano na baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka la Iran.
Queiroz ambaye ni mzaliwa wa Msumbiji amesema  hapendi kuahidi atafanyaje katika timu hiyo ya taifa lakini mikakati yake ni kuiongoza vyema  kwenye michuano ya mataifa ya barani Asia  itakayofanyika mwezi ujao nchini Australia.
Iran ambayo imelitwaa taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 1976 imepangwa kundi C lenye mataifa ya United Arab Emirates, Bahrain  na  Qatar huku kocha Queiroz akiahidi pia kuisaidia nchini Iran kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018

                              Mkule.blogsport.com