Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 3, 2013

ZANZIBAR HEROS YAJITIA KITANZI KATIKA MICHUANO YA CHALLENGE BAADA YA KURARURIWA NA KENYA 2-0.

Timu ya taifa ya Zanzibar Heros leo imejitia gizani kwenye  mashindano ya challange nchini Kenya baada ya kunyukwa magoli 2 bila majibu na timu ya taifa ya Kenya Harambe Stars mchezo uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Afrah mjini Nakuru.


Magoli ya washindi kwenye mchezo huo wa kundi A yametiwa kimiani na mchezaji Joackins Atudo kwa penalti dakika ya sita na mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga kunako  dakika ya 60.

Katika mchezo mwingine uliochezwa leo timu ya soka ya Sudani kusini imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa magoli 2 kwa 0 na Ethiopia pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Afrah uliopo mjini Nakuru.

Magoli ya Ethiopia yamefungwaYousuf Yassin na Biruk Kalbolre.

Sudan kusini imeyaaga mashindano hayo bila kushinda mchezo wowote katika kundi lake la A.


Michuano hiyo inataraji kuendelea tena kesho ambapo timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro stars itakuwa uwanjani kucheza na Burundi huku Somalia ikiikabili Zambia Chipolopo  michezo ambayo itatoa taaswira ya nani ataongoza kundi hilo huku vita kali ikiwa ni kwa Zambia,Burundi  na Kili Stars.

Huu ni msimamo wa kundi B.

Group B

#   Team MP W D L F A D P Last 5 matches H2H
1 Previous rank: 3 2 1 1 0 2 1 +1 4 W D
2 Previous rank: 4 2 1 1 0 2 1 +1 4 W D
3 Previous rank: 1 2 1 0 1 2 1 +1 3 L W
4 Previous rank: 2 2 0 0 2 0 3 -3 0
mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment