Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 4, 2013

SAMATA AIPELEKA ROBO FAINALI KILIMANJARO STARS MICHUANO YA CHALLENGE




Timu ya tifa ya Tanzania bara Kilimanjaro stars imetinga rasmi  robo fainali ya michuano ya Challenge  baada ya leo kuinyuka Burundi goli 1 kwa 0 katika mchezo uliochezwa nchini Kenya.
  
Bao pekee la Kili stars limefungwa na Mbwana Samata dkk 7 nakuifanya timu hiyo kutoka Tanzania bara kuingia moja kwa mmoja hatua mhimu ya michuano hiyo iliyoanza November 27 ikishirikisha mataifa wanachama wa Cecafa.
Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro stars  imemaliza ikiwa na alama  7 baada ya awali kushinda  goli 1-0 dhidi ya Somalia na kutoka sare
ya kufungana goli 1 kwa1 na  mabingwa wa zamani wa Afrika timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo.

Mchezo unaoendelea hivi sasa ni kati ya Somalia ambao wapo nyuma kwa magoli 3 kwa 0 dhidi ya  timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo.
Kwajinsi hali ilivyo uwezekano ni mkubwa mno kwa Zambia kuuungana na Kilimanjaro stars kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo kutoka kunda B.

mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment