Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 3, 2013

UJENZI WA VIWANJA VITATU VITAKAVYOTUMIKA KWENYE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL KUTOKAMILIKA KATIKA MUDA ULIOPANGWA NA FIFA.



 Arena Corinthians

Jumla ya viwanja vitatu kati ya vinavyojengwa nchini Brazil kwaajili ya fainali za kombe la dunia havitakuwa tayari kukamilika katika muda uliopangwa na shirikisho la soka duniani Fifa.

Viwanja hivyo vya Arena Pantanal uliopo kwenye mji wa Cuiaba,Arena da Baixada uliopo Curitiba na Arena Corinthians uliopo Sao Paulo havitakuwa vimekamilika hadi kufikia December 31 Fifa imethibitisha hilo.

Ujenzi wa viwanja vyote vitakavyotumika kwenye fainali za mwakani nchini Brazil unatakiwa kukamilika hadi kufikia tarehe 31 ya mwezi huu pamoja na kukumbwa na maafa ya kuporomoka kwa dhaadhi ya viwanja kiasi cha kupoteza maisha ya watu.

Uwanja uliopo Sao Paulo mwezi uliopita ulisababisha vifo vya watu wawili wanaume waliokuwakwenye ujenzi wa dimba la Arena Corinthians ambalo upo kweenye orodha ya viwanja vitatu vitakavyoshindwa kukamilika katika muda uliopangwa na fifa.

                Arena da Baixada uliopo Curitiba.

                       Arena Pantanal uliopo kwenye mji wa Cuiaba.

                                     mkule.blospot.com

No comments:

Post a Comment