Pages

Ads 468x60px

Tuesday, December 3, 2013

HAUZWI NG'OOOOO,ASISTIZA PELLEGRINI KUWAONYA WANAOMTOLEA UDENDA.





Bosi wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrin amekanusha vikali habari kuwa mshambuliaji Edin Dzeco anaweza kuuzwa mwezi januari mwakani katika msimu wa usajili barani Ulaya.

Katika taarifa yake Pellegrin amesema nyota huyio mwenye umri wa miaka 27 atabakia kuwa mmoja wa watakaoendelea kuitumikia  klabu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester nay eye binafsi hayupo tayari kumpoteza msjhambuliaji huyo.

Pellegrin amesema ni jambo la mhimu sana kwa timu yake kuwa na kikosi imara kwakuwa wanakabiliwa na michezo mingi ya kucheza kwasasa hadi mwezi wan ne mwakani na kama wanahitaji mataji sharti wawe na wachezaji wazuri.
Haya ni maneno ya Pellegrin akisistiza kutompiga bei  Dzeco "Maybe at the moment he is not playing as much as he would like, but he remains an important part of the squad."

Kauli ya kocha huyo alieiwezesha City kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu huu itakuwa ni mwiba mkali kwa mashabiki wa vilabu vya Arsenal, Borussia Dortmund na Inter Milan ambavyovimekuwa katika vita ya kutaka saini yake.


Dzeco amefunga magoli 7 katika michezo 14 aliyocheza msimu huu kwenye mashindano yote lakini amekuwa na mwanzo mbaya msimu huu wa ligi kuu ya England tangu mwishoni mwa mwezi September mwaka huu.

mkule.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment