Pages

Ads 468x60px

Monday, December 2, 2013

YAYA TOURE ATWAA TUZO YA BBC YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA 2013.






Kiungo wa klabu ya soka ya Manchester City na timu ya taifa ya Ivory coast Yaya Toure ametangazwa mshindi wea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka wa 2013 katika tuzo zinazotolewa na shirika la utangazaji la BBC.

Yaya ambaye ameingia katika kinyang’anyiro hicho kwa miaka minne amewashinda wachezaji Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na  Jonathan Pitroipa  ambao wote kwa pamoja wameshindwa kutamba mbele yake.

Akizungumza mara baada ya kupata tuzo hiyo Yaya mwenye umri wa miaka 30 hivi sasa amesema amefarijika sana kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya kuingizwa kwenye kinyang’anyiri hicho mara nne bila mafanikio lakini mara ya tano amekuwa mshindi.

Ameongeza kuwa ni mafanikio makubwa kwake kuwa mchezaji bora wa Afrika akiwaburuza nyota wa kiafrika kama Aubameyang, Pitroipa, Mikel, Moses, Salomon Kalou, Gervinho ambao kwasasa wanatamba katika soka la kimataifa.

Wafuatao ni wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo miaka iliyopita;-
  • 2012 - Christopher Katongo (Zambia and Henan Construction)
  • 2011 - Andre 'Dede' Ayew (Marseille & Ghana)
  • 2010 - Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)
  • 2009 - Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
  • 2008 - Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)
  • 2007 - Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
  • 2006 - Michael Essien (Chelsea & Ghana)
  • 2005 - Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)
  • 2004 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
  • 2003 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
  • 2002 - El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
  • 2001 - Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
  • 2000 - Patrick Mboma (Parma & Cameroon)
Mbali na kutoa mchango mkubwa kwa klabu yake ya Manchester City kwenye ligi kuuu ya England na katika michuano ya klabu bingwa Ulaya Yaya amekuwa msaada mkubwa kuiwezesha Ivory Coast kuwa miongoni mwa mataifa matano ya Afrika yatakayoshiriki fainali zijazo za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment