Kikosi
cha wachezaji 20 na viongozi tisa cha timu ya Tanzania ya wasichana chini ya
miaka 20 (Tanzanite) kimewasili leo jijini Johannesburg tayari kwa mechi dhidi
ya wenyeji Afrika Kusini (Batsesana).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe
la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani
nchini Canada.
Tanzanite
imefikia Millpark Garden Court Hotel tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa
Jumamosi katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa
9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini.
Wachezaji
wa Tanzanite walioko katika kikosi hicho ni Amina Bilali, Amina Hemed, Amisa
Hussein, Anastaz Katunzi, Anna Mwaisula, Belina Nyamwihula, Donisia Minja,
Fatuma Maonyo, Happiness Mwaipaja, Latifa Salum, Maimuna Kaimu, Najiat Idrisa,
Neema Kiniga, Rehema Rhamia, Sada Hussein, Shelda Mafuru, Stumai Athuman, Tatu
Salum, Theresa Kashilim na Vumilia Maarifa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.
No comments:
Post a Comment