Kikosi
cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana
wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini
Alhamisi (Desemba 5 mwaka huu).
Afrika
Kusini ambayo itafikia hoteli ya Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa
Airways.
Mechi hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo
kutoka Uganda wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Gebreyohanis Trhas kutoka
Ethiopia. Waamuzi wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto Nkumbi na Irene
Namubiru.
Kamishna wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia.
Muinjo pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na mjumbe wa
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF).
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi
(Desemba 7 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa
VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea
na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa
mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu
mkoani Pwani.
Boniface
Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu
Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
mkule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment