TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba
26, 2013
Mechi
ya kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kati ya Azam na Ruvu Shooting
inachezwa leo (Desemba 26 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Chamazi, Dar
es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo ya majaribio ni sh. 1,000
na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB
Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kitakapoanza kipindi cha pili.
Mawakala
18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora,
Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa
Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment
Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.
Ghomme
Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni,
K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB
Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly
Investment Company Limited.
Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo,
S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry
Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz
Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko, .
Mechi nyingine ya majaribio itakuwa kati ya Ashanti
United na JKT Ruvu ambayo itachezwa Januari Mosi mwakani kwenye uwanja huo huo.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na
Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF)
No comments:
Post a Comment