Desemba 13, 2013
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa
ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika.
Mipira hiyo 250 yenye thamani ya sh.
16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira
mmoja una thamani y ash. 65,000.
Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo
itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.
MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA
JUMAPILI
Robo ya mwisho ya mitihani ya
waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa mwaka
2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili (Desemba 15 mwaka huu).
Mitihani hiyo inayofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi wenye beji za Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa kundi la waamuzi (elite) ambao
wanaweza kupendekezwa kupewa beji za FIFA.
Wakufunzi wa mitihani hiyo ya
waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Waamuzi wa FIFA watakaofanya
mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse
Erasmus, John Kanyenye, Josephat Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan
Ibada, Samwel Mpenzu na Waziri Sheha.
Washiriki kutoka kundi la elite ni
Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma, Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth
Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba, Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro
na Mohamed Mkono.
KILIMANJARO
STARS YAREJEA DAR
Timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji
iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es Salaam leo.
Kilimanjaro
Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa ndege ya RwandAir.
Wenyeji
Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya
kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana Uwanja wa
Nyayo.
Boniface
Wambura Mgoyo
Kaimu
Katibu Mkuu
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF
No comments:
Post a Comment