Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 7, 2013

KILI STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA CHALLENGE.



Timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars leo imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Challenge baada ya kuwaondosha mabingwa watetezu Uganda kwa mikwaju ya Penalti  3 kwa 2 kufuatia timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2 kwa 2 katika muda wa dkk 90.

Katika mchezo huo Penati za Kili Stars zimefungwa na Othman Idd Chuji,Amri Kiemba na Kelvin Yondan huku Erasto Nyoni mkwaju wake ukigonga mtambaa panya na Mbwana Samata mkwaju wake ukidakwa na mlindamlango wa Uganda.

Kwa upande wa Uganda penalty zao mbili zimefungwa na Hamisi Kiiza na Emanuel Okwi huku  penalti zao 2 zikizuiliwa na Ivo Mapunda na mmoja ikipaa juu ya lango.

 Kili Stars ilipata pigo dakika ya 53 baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa nyekundu kwa kumchezea rafu Sserunkuma.
Uganda ikapata bao la kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Martin Mpuga, aliyeunganisha kona ya Godfrey Walusimbi.
Baada ya mchezo kumalizika nyota wa mchezo huo "man of the match".

Robo fainali ya pili leo.

Kenya 1 vs 0 Rwanda. Mfungaji…Joackins Atudo kwa penalti dakika ya 56.

KESHO;-
Zambia vs Burundi.
Ethiopia vs Sudani.

TANZANITE YACHAPWA 4 - 1 NA AFRIKA YA KUSINI.

Timu ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 Tanzanite leo imebugizwa magoli 4 kwa 1 na timu ya taifa ya Afrika ya kusini  katika pambano la kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Canada.
akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha mkuu wa kikosi cha Tanzanite Rogasiani Kaijage mbali na kukuri kupata kipigo cha halali lakini amesema bado kunamatumaini ya kulipa kisasi kwenye pambano la marejeano siku chache zijazo.
Naye mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho la soka nchini Saadi Kawemba amesema kipigo hicho kimewasikitisha watanzia wengi lakini wanasubiri taarifa ya benchi la ufundi na baada ya mchezo wa leo wamepanga kuipa timu hiyo maandalizi ya kutosha.

mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment