Pages

Ads 468x60px

Saturday, April 5, 2014

BAYER LEVERKUSEN YAMTUPIA VIRAGO KOCHA SAMI HYYPIA.



Uongozi wa timu ya soka ya Bayer Leverkusen ya Ujeruman umetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Sami Hyypia kufuatia timu hiyo kubugizwa magoli 2 kwa1 na Lowly Hamburg.

Uamuzi wa kumtupia virago kocha huyo unatokana na mwenendo mbaya wa timu ambapo katika michezo 14 imeshinda michezo 3 pekee pamoja na kipigo cha jana ijumaa dhidi ya Lowly Hamburg.

Matokeo ya jana yamezidi kuiweka pabaya timu hiyo katika kukata tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao  na badala yake  nafasi ya kushiriki Uefa msimu ujao huenda ikaangukia kwa Wolfsburg  na Borussia Monchengladbach endapo timu hizo zitashinda michezo waliyonayo mwishoni mwa juma hili.

Hyypia ambae alianza kuinoa Leverkusen mwezi mei 2012 taarifa zimeeleza kuwa nafasi yake huenda ikachukuliwa na kocha wa timu ya vijana Sascha Lewandowski ambae atakuwa akimalizia michezo ya msimu huu wa Bundesiliga.

 Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 40 mkataba wake wasasa ndani ya timu ya Leverkusen ulikuwa unamalizika katika msimu wa ligi mwaka 2015.
Posted by Yusuph Mkule. 

PIGO MAN UNITED,ROONEY HATARINI KUIKOSA MECHI DHIDI YA FC BAYERN MUNICH...



 

Timu ya Manchester United ya nchini England ipo kwenye hatihati ya kumkosa mshambuliaji wake Wayne Rooney katika mchezo wa marudiano dhidi ya Bayern Munich kuwania ubingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu.


Taarifa iliyotolewa na kocha mkuu wa timu hiyo David Moyes imesema kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amepata jeraha na kidole gumba cha mguu jeraha linalotishia kuukosa mchezo huo wa robo fainali.

Kwamujibu wa kocha huyo Rooney ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Newcastle United kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England ambapo Manchester United imekuwa na msimu mbaya kiasi cha kusota kwenye nafasi ya saba hadi sasa.


Rooney ambaye amefunga magoli thelathini kwenye michezo themanini na moja anataraji kupatiwa matibabu mwishoni mwa juma hili ili kuona kama ataweza kucheza dhidi ya Bayern Munich.

posted by Yusuph Mkule.