Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 13, 2013

KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA LIGI KUU YA ENGLAND MSIMU HUU WA 2013/2014 KUANZA KUTUMIA GOAL LINE TECHNOLOGY.


Kwa mara ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya England teknolojia ya kutambua kama mpira umeingia golini inataraji kuanza kutumika  msimu huu wa 2013/2014 itatumia kifaa hicho.

Uamuzi wa kupitisha kifaa hicho kitumike kwaajili ya kuondoa malalamiko yaliyokuwa yanajitokeza katika baadhi ya magoli misimu kadhaa iliyopita umefikiwa kufuatia kifaa hicho kijulikancho kama Hawk-Eye kupitishwa mwezi wa nne mwaka huu.

Kifaa hicho kilichotengenezwa na kampuni moja ya nchini Ujeruman kimaonyesha matokeo mazuri katika majaribio yake na kimetumika kwenye fainali za kombe la mabara mwaka huu zilizofanyika nchini Brazil.



Teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye michezo ya ligi msimu wa 2013/2014 inayotaraji kuanza jumamosi ya wiki hii na kuwa ligi ya kwanza kwa mataifa ya Ulaya kuanza kutumia kifaa hicho kilichoanza kujaribiwa tangu mwaka 2006.