Nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Arsenal Mesut
Ozil ameondolewa kwenye kikosi cha kocha Joaquim Low kitakacho ikabili England
hapo kesho kwenye mcchezo wa kirafiki wa kimataifa kwamujibu wa kaenda za fifa.
Ozil ameondolewa kwenye orodha ya weachezaji
watakaocheza mchezo huo kutoakana na kusumbuliwa na jeraha ambalo alilipata
katika mchezo baina ya Ujerumani na Italia uliochezwa ijumaa iliyopita na
kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1.
Kukosekana kwa Ozil ni pigo jingine kwa kocha
wa Ujerumani baada ya kiungo Sami Khedira kuumia goti kwenye mchezo uliopita wa kirafiki
nakuelezwa kuwa atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita na anatarajiwa
kufanyiwa upasuaji.
Katika mchezo na Italia Ozil aliingia dakika ya 59 na nafasi kuchukua nafasi ya Mario Gotze pambano ambalo Ujerumani ilitawala
kwa kiwango kikubwa.
Katika hatua nyingine timu ya taifa ya
England huenda ikamkosa mshambuliaji wake Daniel Sturridge kwenye mchezo huo
baada ya hii leo kuondoka mazoezini kwakile kinachodhaniwa kuumia akiwa
mazoezini.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment